Lyrics

Zipo sheria pia amri za barabarani zitupasazo kuzitii tukiwa safarini, kinachoshangaza muda mwingi tunasahau kuwa hizo amri zipo kwa usalama wetu, ndio sababu unawaona madereva wakiendesha kwa kuchungana na polisi, mwendo mkali bila kujali chochote, maisha yake hata maisha ya wengine, pale atapoona askari kwa mbali atajifanya kuzijali amri na sheria kusudi ampendeze askari huyo ila sio kwamba ajiepushe na ajali, ivyo divyo ilivyo sheria ya Mungu iko kwa usalama wetu Mungu mwenyewe aimsaidii kwalolote ila nikwa faida yetu lakini siku hizi za mwisho yapo mafundisho yaa kwamba amri zake Mungu hazifai tena usidanganyike ndugu msafiri mwenzangu bila amri ya Mungu atutafika salamaaaa. Katika safari hii ya wokovu twahitaji mwongozo tuwekwe sawa na jamii ya mbinguni kama ni kweli twaudhamini wokovu ule basi tutazishika amri kwa usafi wetu, kama ni kuiba madhara yake twayajua jeee kuzini matunda yake yako wazi usidanganye kumbuka pale ulipodanganya na jinsi ulikovyosa amani moyoni jambo hili li wazi kwamba jamii iliyo yote huwa na utamaduni pia desturi yake kwahiyo kazi yake amri na ile sheria ni kutuzoeza na utamaduni wa mbinguni. Dalili moja kwabma unampenda Bwana utawafundisha watu kuzitii amri zake hata Bwana mwenyewe kwa kinywa chake asema kama kweli mwanipenda mtaztii amri zangu, hivo yatupasa wote tulokombolewa kujizoeza nayo desturi ya nyumbani punde safari itafikia mwisho wake, anayo heri atakayefikia salama wewe uhubirie neno ni kama dereva tena wale wafuasi wako ni abiria wapaswa kuzidhamini sheria za huku njiani ili ufike salama na abiria .
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out